9 Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari.Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.
10 Ndiwe uliyemseta Rahabu akawa kama aliyeuawa,Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao.
11 Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako,Ulimwengu na vyote viujazavyoNdiwe uliyeupiga msingi wake.
12 Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba,Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13 Mkono wako ni mkono wenye uweza,Mkono wako una nguvu,Mkono wako wa kuume umetukuka.
14 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako,Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.
15 Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe,Ee BWANA, huenenda katika nuru ya uso wako.