1 Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote;Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;
2 Nitafurahi na kukushangilia Wewe;Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu.
3 Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma;Hujikwaa na kuangamia mbele zako.
4 Kwa maana umenifanyia hukumu na hakiUmeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki.