12 Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka,Hakukisahau kilio cha wanyonge.
13 Wewe, BWANA, unifadhili,Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia;Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,
14 Ili nizisimulie sifa zako zote;Katika malango ya binti SayuniNitaufurahia wokovu wako.
15 Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya;Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.
16 BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu;Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.
17 Wadhalimu watarejea kuzimu,Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
18 Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima;Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.