16 BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu;Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.
17 Wadhalimu watarejea kuzimu,Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
18 Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima;Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele.
19 BWANA, usimame, mwanadamu asipate nguvu,Mataifa wahukumiwe mbele zako.