4 Kwa maana umenifanyia hukumu na hakiUmeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki.
5 Umewakemea mataifa;Na kumwangamiza mdhalimu;Umelifuta jina lao milele na milele;
6 Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele.Nayo miji yao uliing’oa;Hata kumbukumbu lao limepotea.
7 Bali BWANA atakaa milele,Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.
8 Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki;Atawaamua watu kwa adili.
9 BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa,Naam, ngome kwa nyakati za shida.
10 Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe,Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.