1 Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu,Kizazi baada ya kizazi.
2 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3 Wamrudisha mtu mavumbini,usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4 Maana miaka elfu machoni pakoNi kama siku ya jana ikiisha kupita,Na kama kesha la usiku.
5 Wawagharikisha, huwa kama usingizi,Asubuhi huwa kama majani yameayo.