3 Wamrudisha mtu mavumbini,usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4 Maana miaka elfu machoni pakoNi kama siku ya jana ikiisha kupita,Na kama kesha la usiku.
5 Wawagharikisha, huwa kama usingizi,Asubuhi huwa kama majani yameayo.
6 Asubuhi yachipuka na kumea,Jioni yakatika na kukauka.
7 Maana tumetoweshwa kwa hasira yako,Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.
8 Umeyaweka maovu yetu mbele zako,Siri zetu katika mwanga wa uso wako.
9 Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako,Tumetowesha miaka yetu kama kite.