1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juuAtakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku,Wala mshale urukao mchana,