3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku,Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani,Wala uele uharibuo adhuhuri,
7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako.Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume!Hata hivyo hautakukaribia wewe.
8 Ila kwa macho yako utatazama,Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9 Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.