1 Ni neno jema kumshukuru BWANA,Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.
2 Kuzitangaza rehema zako asubuhi,Na uaminifu wako wakati wa usiku.
3 Kwa chombo chenye nyuzi kumi,Na kwa kinanda,Na kwa mlio wa kinubi.
4 Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA,Kwa kazi yako; nitashangiliaKwa ajili ya matendo ya mikono yako.
5 Ee BWANA, jinsi yalivyo makuu matendo yako!Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
6 Mtu mjinga hayatambui hayo,Wala mpumbavu hayafahamu.