4 Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA,Kwa kazi yako; nitashangiliaKwa ajili ya matendo ya mikono yako.
5 Ee BWANA, jinsi yalivyo makuu matendo yako!Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
6 Mtu mjinga hayatambui hayo,Wala mpumbavu hayafahamu.
7 Wasio haki wakichipuka kama majaniNa wote watendao maovu wakistawi.Ni kwa kusudi waangamizwe milele;
8 Bali Wewe, BWANA, U Mtukufu hata milele.
9 Maana hao adui zako, Ee BWANA,Hao adui zako watapotea,Na watendao maovu watatawanyika wote pia.
10 Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati,Nimepakwa mafuta mabichi.