9 Maana hao adui zako, Ee BWANA,Hao adui zako watapotea,Na watendao maovu watatawanyika wote pia.
10 Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati,Nimepakwa mafuta mabichi.
11 Na jicho langu limewatazama walioniotea,Sikio langu limesikia habari za waovu walionishambulia.
12 Mwenye haki atasitawi kama mtende,Atakua kama mwerezi wa Lebanoni.
13 Waliopandwa katika nyumba ya BWANAWatasitawi katika nyua za Mungu wetu.
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee,Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.