1 Ee BWANA, Mungu wa kisasi,Mungu wa kisasi, uangaze,
2 Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze,Uwape wenye kiburi stahili zao.
3 BWANA, hata lini wasio haki,Hata lini wasio haki watashangilia?
4 Je! Wote watendao uovu watatoa maneno,Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?
5 Ee BWANA, wanawaseta watu wako;Wanautesa urithi wako;
6 Wanamwua mjane na mgeni;Wanawafisha yatima.
7 Nao husema, BWANA haoni;Mungu wa Yakobo hafikiri.