2 Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze,Uwape wenye kiburi stahili zao.
3 BWANA, hata lini wasio haki,Hata lini wasio haki watashangilia?
4 Je! Wote watendao uovu watatoa maneno,Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?
5 Ee BWANA, wanawaseta watu wako;Wanautesa urithi wako;
6 Wanamwua mjane na mgeni;Wanawafisha yatima.
7 Nao husema, BWANA haoni;Mungu wa Yakobo hafikiri.
8 Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini;Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?