5 Ee BWANA, wanawaseta watu wako;Wanautesa urithi wako;
6 Wanamwua mjane na mgeni;Wanawafisha yatima.
7 Nao husema, BWANA haoni;Mungu wa Yakobo hafikiri.
8 Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini;Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?
9 Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?Aliyelifanya jicho asione?
10 Awaadibuye mataifa asikemee?Amfundishaye mwanadamu asijue?
11 BWANA anajua mawazo ya mwanadamu,Ya kuwa ni ubatili.