9 Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?Aliyelifanya jicho asione?
10 Awaadibuye mataifa asikemee?Amfundishaye mwanadamu asijue?
11 BWANA anajua mawazo ya mwanadamu,Ya kuwa ni ubatili.
12 Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye,Na kumfundisha kwa sheria yako;
13 Upate kumstarehesha siku za mabaya,Hata asiye haki atakapochimbiwa shimo.
14 Kwa kuwa BWANA hatawatupa watu wake,Wala hutauacha urithi wake,
15 Maana hukumu itairejea haki,Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.