1 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Mwimbieni BWANA, nchi yote.
2 Mwimbieni BWANA, libarikini jina lake,Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,Na watu wote habari za maajabu yake.
4 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana.Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
5 Maana miungu yote ya watu si kitu,Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
6 Heshima na adhama ziko mbele zake,Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.