2 Mwimbieni BWANA, libarikini jina lake,Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,Na watu wote habari za maajabu yake.
4 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana.Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
5 Maana miungu yote ya watu si kitu,Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
6 Heshima na adhama ziko mbele zake,Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
7 Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
8 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake,Leteni sadaka mkaziingie nyua zake.