5 Maana miungu yote ya watu si kitu,Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
6 Heshima na adhama ziko mbele zake,Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
7 Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
8 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake,Leteni sadaka mkaziingie nyua zake.
9 Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu,Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
10 Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki;Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike,Atawahukumu watu kwa adili.
11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,Bahari na ivume na vyote viijazavyo,