9 Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu,Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
10 Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki;Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike,Atawahukumu watu kwa adili.
11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
12 Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo,Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;