1 BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
2 BWANA katika Sayuni ni mkuu,Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
3 Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa;Ndiye mtakatifu.
4 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu;Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili;Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.