8 Hukaa katika maoteo ya vijiji.Mahali pa siri humwua asiye na hatia,Macho yake humvizia mtu duni.
9 Huotea faraghani kama simba pangoni,Huotea amkamate mtu mnyonge.Naam, humkamata mtu mnyonge,Akimkokota wavuni mwake.
10 Hujikunyata na kuinama;Watu duni huanguka kwa nguvu zake.
11 Asema moyoni mwake, Mungu amesahau,Auficha uso wake, haoni kamwe.
12 BWANA, uondoke, Ee Mungu, uuinue mkono wako,Usiwasahau wanyonge.
13 Kwani mdhalimu kumdharau Mungu.Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza?
14 Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri,Uyatwae mkononi mwako.Mtu duni hukuachia nafsi yake,Maana umekuwa msaidizi wa yatima.