1 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.Wewe, BWANA, Mungu wangu,Umejifanya mkuu sana;Umejivika heshima na adhama.
2 Umejivika nuru kama vazi;Umezitandika mbingu kama pazia;
3 Na kuziweka nguzo za orofa zake majini.Huyafanya mawingu kuwa gari lake,Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,
4 Huwafanya malaika zake kuwa pepo,Na watumishi wake kuwa moto wa miali.
5 Uliiweka nchi juu ya misingi yake,Isitikisike milele.