35 Bali walijichanganya na mataifa,Wakajifunza matendo yao.
36 Wakazitumikia sanamu zao,Nazo zikawa mtego kwao.
37 Naam, walitoa wana wao na binti zaoKuwa dhabihu kwa mashetani.
38 Wakamwaga damu isiyo na hatia,Damu ya wana wao na binti zao,Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani;Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.
39 Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao,Wakafanya uasherati kwa matendo yao.
40 Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake,Akauchukia urithi wake.
41 Akawatia mikononi mwa mataifa,Nao waliowachukia wakawatawala.