39 Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao,Wakafanya uasherati kwa matendo yao.
40 Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake,Akauchukia urithi wake.
41 Akawatia mikononi mwa mataifa,Nao waliowachukia wakawatawala.
42 Adui zao wakawaonea,Wakatiishwa chini ya mkono wao.
43 Mara nyingi aliwaponya,Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao,Wakadhilika katika uovu wao.
44 Lakini aliyaangalia mateso yao,Aliposikia kilio chao.
45 Akawakumbukia agano lake;Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;