1 BWANA, uokoe, maana mcha Mungu amekoma,Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
2 Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe,Wenye midomo ya kujipendekeza;Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
3 BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;
4 Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda;Midomo yetu ni yetu wenyewe,Ni nani aliye bwana juu yetu?
5 Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge,Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji,Sasa nitasimama, asema BWANA,Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
6 Maneno ya BWANA ni maneno safi,Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi;Iliyosafishwa mara saba.
7 Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi,Utatulinda na kizazi hiki milele.