5 Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe,Mkono wangu wa kuume na usahau.
6 Ulimi wangu na ugandamaneNa kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka.Nisipoikuza YerusalemuZaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
7 Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu,Siku ya Yerusalemu.Waliosema, Bomoeni!Bomoeni hata misingini!
8 Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia,Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.