1 Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu,Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako.
2 Wala usimhukumu mtumishi wako,Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.
3 Maana adui ameifuatia nafsi yangu,Ameutupa chini uzima wangu.Amenikalisha mahali penye giza,Kama watu waliokufa zamani.
4 Na roho yangu imezimia ndani yangu,Moyo wangu ndani yangu umesituka.
5 Nimezikumbuka siku za kale,Nimeyatafakari matendo yako yote,Naziwaza kazi za mikono yako.
6 Nakunyoshea mikono yangu;Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.