1 Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana;
2 BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
3 Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa,Hivyo nitaokoka na adui zangu.
4 Kamba za mauti zilinizunguka,Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.
5 Kamba za kuzimu zilinizunguka,Mitego ya mauti ikanikabili.
6 Katika shida yangu nalimwita BWANA,Na kumlalamikia Mungu wangu.Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.