4 Sauti yao imeenea duniani mwote,Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.Katika hizo ameliwekea jua hema,
5 Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake,Lafurahi kama mtu aliye hodariKwenda mbio katika njia yake.
6 Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu,Na kuzunguka kwake hata miisho yake,Wala kwa hari yakeHakuna kitu kilichositirika.
7 Sheria ya BWANA ni kamilifu,Huiburudisha nafsi.Ushuhuda wa BWANA ni amini,Humtia mjinga hekima.
8 Maagizo ya BWANA ni ya adili,Huufurahisha moyo.Amri ya BWANA ni safi,Huyatia macho nuru.
9 Kicho cha BWANA ni kitakatifu,Kinadumu milele.Hukumu za BWANA ni kweli,Zina haki kabisa.
10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu,Kuliko wingi wa dhahabu safi.Nazo ni tamu kuliko asali,Kuliko sega la asali.