7 Sheria ya BWANA ni kamilifu,Huiburudisha nafsi.Ushuhuda wa BWANA ni amini,Humtia mjinga hekima.
8 Maagizo ya BWANA ni ya adili,Huufurahisha moyo.Amri ya BWANA ni safi,Huyatia macho nuru.
9 Kicho cha BWANA ni kitakatifu,Kinadumu milele.Hukumu za BWANA ni kweli,Zina haki kabisa.
10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu,Kuliko wingi wa dhahabu safi.Nazo ni tamu kuliko asali,Kuliko sega la asali.
11 Tena mtumishi wako huonywa kwazo,Katika kuzishika kuna thawabu nyingi.
12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake?Unitakase na mambo ya siri.
13 Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi,Yasinitawale mimi.Ndipo nitakapokuwa kamili,Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.