1 BWANA akujibu siku ya dhiki,Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.
2 Akupelekee msaada toka patakatifu pake,Na kukutegemeza toka Sayuni.
3 Azikumbuke sadaka zako zote,Na kuzitakabali dhabihu zako.
4 Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako,Na kuyatimiza mashauri yako yote.
5 Na tuushangilie wokovu wako,Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu.BWANA akutimizie matakwa yako yote.
6 Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake;Atamjibu toka mbingu zake takatifu,Kwa matendo makuu ya wokovuYa mkono wake wa kuume.
7 Hawa wanataja magari na hawa farasi,Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.