1 BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,Nimwogope nani?BWANA ni ngome ya uzima wangu,Nimhofu nani?
2 Watenda mabaya waliponikaribia,Wanile nyama yangu,Watesi wangu na adui zangu,Walijikwaa wakaanguka.
3 Jeshi lijapojipanga kupigana nami,Moyo wangu hautaogopa.Vita vijaponitokea,Hata hapo nitatumaini.
4 Neno Moja nimelitaka kwa BWANA,Nalo ndilo nitakalolitafuta,Nikae nyumbani mwa BWANASiku zote za maisha yangu,Niutazame uzuri wa BWANA,Na kutafakari hekaluni mwake.
5 Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya,Atanisitiri katika sitara ya hema yake,Na kuniinua juu ya mwamba.
6 Na sasa kichwa changu kitainukaJuu ya adui zangu wanaonizunguka.Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake;Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
7 Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia,Unifadhili, unijibu.