6 Na sasa kichwa changu kitainukaJuu ya adui zangu wanaonizunguka.Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake;Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
7 Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia,Unifadhili, unijibu.
8 Uliposema, Nitafuteni uso wangu,Moyo wangu umekuambia,BWANA, uso wako nitautafuta.
9 Usinifiche uso wako,Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira.Umekuwa msaada wangu, usinitupe,Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
10 Baba yangu na mama yangu wameniacha,Bali BWANA atanikaribisha kwake.
11 Ee BWANA, unifundishe njia yako,Na kuniongoza katika njia iliyonyoka;Kwa sababu yao wanaoniotea;
12 Usinitie katika nia ya watesi wangu;Maana mashahidi wa uongo wameniondokea,Nao watoao jeuri kama pumzi.