13 Maana nimesikia masingizio ya wengi;Hofu ziko pande zote.Waliposhauriana juu yangu,Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
14 Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA,Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
15 Nyakati zangu zimo mikononi mwako;Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.
16 Umwangaze mtumishi wakoKwa nuru ya uso wako;Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
17 Ee BWANA, nisiaibishwe, maana nimekuita;Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.
18 Midomo ya uongo iwe na ububu,Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi,Kwa majivuno na dharau.
19 Jinsi zilivyo nyingi fadhili zakoUlizowawekea wakuchao;Ulizowatendea wakukimbiliaoMbele ya wanadamu!