6 Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo;Bali mimi namtumaini BWANA.
7 Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako,Kwa kuwa umeyaona mateso yangu.Umeijua nafsi yangu taabuni,
8 Wala hukunitia mikononi mwa adui;Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi.
9 Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki,Jicho langu limenyauka kwa masumbufu,Naam, mwili wangu na nafsi yangu.
10 Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni,Na miaka yangu kwa kuugua.Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu,Na mifupa yangu imekauka.
11 Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu,Naam, hasa kwa jirani zangu;Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu;Walioniona njiani walinikimbia.
12 Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa;Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.