4 Waaibishwe, wafedheheshwe,Wanaoitafuta nafsi yangu.Warudishwe nyuma, wafadhaishwe,Wanaonizulia mabaya.
5 Wawe kama makapi mbele ya upepo,Malaika wa BWANA akiwaangusha chini.
6 Njia yao na iwe giza na utelezi,Malaika wa BWANA akiwafuatia.
7 Maana bila sababu wamenifichia wavu,Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.
8 Uharibifu na umpate kwa ghafula,Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe;Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
9 Na nafsi yangu itamfurahia BWANA,Na kuushangilia wokovu wake.
10 Mifupa yangu yote itasema,BWANA, ni nani aliye kama Wewe?Umponyaye maskini na mtu aliye hodari kumshinda yeye,Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.