1 Nalisema, Nitazitunza njia zanguNisije nikakosa kwa ulimi wangu;Nitajitia lijamu kinywani,Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.
2 Nalikuwa sisemi, nalinyamaa kimya,Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.
3 Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;Nalisema kwa ulimi wangu,
4 BWANA, unijulishe mwisho wangu,Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani;Nijue jinsi nilivyo dhaifu.