9 Nimenyamaza, sitafumbua kinywa changu,Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.
10 Uniondolee pigo lako;Kwa uadui wa mkono wako nimeangamia.
11 Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake,Watowesha uzuri wake kama nondo.Kila mwanadamu ni ubatili.
12 Ee BWANA, usikie maombi yangu,Utege sikio lako niliapo,Usiyanyamalie machozi yangu.Kwa maana mimi ni mgeni wako,Msafiri kama baba zangu wote.