1 Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetuBaba zetu wametuambia,Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
2 Wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa,Ukawakalisha wao.Wewe uliwatesa watu wa nchi,Ukawaeneza wao.
3 Maana si kwa upanga wao walivyoimiliki nchi,Wala si mkono wao uliowaokoa;Bali mkono wako wa kuume, naam, mkono wako,Na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwaridhia.
4 Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu,Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.
5 Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu;Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.
6 Maana sitautumainia upinde wangu,Wala upanga wangu hautaniokoa.
7 Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;Na watuchukiao umewaaibisha.