4 Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu,Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.
5 Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu;Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.
6 Maana sitautumainia upinde wangu,Wala upanga wangu hautaniokoa.
7 Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;Na watuchukiao umewaaibisha.
8 Tumejisifia Mungu mchana kutwa,Na jina lako tutalishukuru milele.
9 Lakini umetutupa, umetufedhehesha,Wala hutoki na majeshi yetu.
10 Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,Na watuchukiao wanajipatia mateka.