1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza,Hakuna atendaye mema.
2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu,Aone kama yuko mtu mwenye akili,Amtafutaye Mungu.
3 Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja,Hakuna atendaye mema,La! Hata mmoja.
4 Je! Wafanyao maovu hawajui?Walao watu wangu kama walavyo mkate,Hawakumwita MUNGU.