1 Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe,Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
2 Ee Mungu, uyasikie maombi yangu,Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3 Kwa maana wageni wamenishambulia;Watu watishao wananitafuta nafsi yangu;Hawakumweka Mungu mbele yao.
4 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.