1 Ee Mungu, umetutupa na kututawanya,Umekuwa na hasira, uturudishe tena.
2 Umeitetemesha nchi na kuipasua,Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.
3 Umewaonyesha watu wako mazito,Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.
4 Umewapa wakuogopao bendera,Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.