1 Ee Mungu, umetutupa na kututawanya,Umekuwa na hasira, uturudishe tena.
2 Umeitetemesha nchi na kuipasua,Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.
3 Umewaonyesha watu wako mazito,Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.
4 Umewapa wakuogopao bendera,Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.
5 Ili wapenzi wako waopolewe,Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie.
6 Mungu amenena kwa utakatifu wake,Nami nitashangilia.Nitaigawanya Shekemu,Nitalipima bonde la Sukothi.
7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,