1 Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,Nafsi yangu inakuonea kiu,Mwili wangu wakuonea shauku,Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
2 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,Nizione nguvu zako na utukufu wako.
3 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;Midomo yangu itakusifu.
4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.