1 Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika,Nao wamchukiao huukimbia uso wake.
2 Kama moshi upeperushwavyo,Ndivyo uwapeperushavyo wao;Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto,Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.
3 Bali wenye haki hufurahi,Na kuushangilia uso wa Mungu,Naam, hupiga kelele kwa furaha.
4 Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,Mtengenezeeni njia ya barabara,Apitaye majangwani kama mpanda farasi;Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.