14 Mwenyezi Mungu alipotawanya wafalme huko,Kulinyesha theluji katika Salmoni.
15 Ni mlima wa Mungu mlima Bashani,Ni mlima mrefu mlima Bashani.
16 Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivuMlima alioutamani Mungu akae juu yake?Naam, BWANA atakaa juu yake milele.
17 Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu;Bwana yumo kati yao kama katika Sinai,Katika patakatifu.
18 Wewe umepaa juu, umeteka mateka,Umepewa vipawa katikati ya wanadamu;Naam, hata na wakaidi, BWANA Mungu akae nao.
19 Na ahimidiwe Bwana,Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;Mungu ndiye wokovu wetu.
20 Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.