18 Wewe umepaa juu, umeteka mateka,Umepewa vipawa katikati ya wanadamu;Naam, hata na wakaidi, BWANA Mungu akae nao.
19 Na ahimidiwe Bwana,Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;Mungu ndiye wokovu wetu.
20 Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.
21 Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake,Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa.
22 Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha,Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari;
23 Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako,Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake.
24 Ee Mungu, wameiona miendo yako;Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu