2 Kama moshi upeperushwavyo,Ndivyo uwapeperushavyo wao;Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto,Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.
3 Bali wenye haki hufurahi,Na kuushangilia uso wa Mungu,Naam, hupiga kelele kwa furaha.
4 Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,Mtengenezeeni njia ya barabara,Apitaye majangwani kama mpanda farasi;Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.
5 Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,Mungu katika kao lake takatifu.
6 Mungu huwakalisha wapweke nyumbani;Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa;Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.
7 Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako,Ulipopita nyikani,
8 Nchi ilitetemekaNaam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu;Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.